Free delivery in Nairobi CBD · Free drop-off to your courier · Countrywide within 24 hours

Hereni za Mifugo Kenya – Ng’ombe, Kondoo, Mbuzi na Nguruwe

Hereni za masikio (ear tags) hukusaidia kutambua kila mnyama na kutunza kumbukumbu za uzalishaji, chanjo, maziwa na uzito. Tunauza hereni zenye namba au zilizochapishwa jina la shamba lako, za ukubwa tofauti, Z-tags na applicator ya kuzifunga.

Bei za hereni za mifugo

Bei za hereni kwa Mkulima Jovial: KSh 35 hadi KSh 2,800 (aina 6, bei zimekaguliwa 13 Novemba 2026). Usafirishaji bure ndani ya Nairobi CBD na hadi kwa courier wako; tunasafirisha kote nchini ndani ya saa 24.

Agiza kwa WhatsApp

Lipa ukipokea – popote Kenya

  1. Agiza mtandaoni na uchague kituo chetu cha kuchukulia mizigo kilicho karibu nawe (vituo 90+ kote nchini).
  2. Lipa ada ndogo kwa M-Pesa: KSh 250 kwa hereni zenye namba na applicator, au KSh 1,000 kwa hereni zilizochapishwa jina lako.
  3. Chukua mzigo na ulipe salio kwa M-Pesa kwenye kituo. Utatumiwa SMS yenye namba ya kuchukua mzigo; mzigo hukaa kituoni siku 7. Usipouchukua ndani ya siku 7, mzigo unarudishwa kwetu na ada ya awali hairudishwi.

Ada ya usafiri huongezwa kwenye salio. Bei: hereni za ng’ombe KSh 2,800 kwa pakiti ya 100 (saizi ya kati); kondoo, mbuzi na nguruwe KSh 2,500 kwa pakiti ya 100. Hereni zilizochapishwa: KSh 50 kwa ng’ombe, KSh 35 kwa kondoo, mbuzi na nguruwe – hakuna kiwango cha chini. Rangi: nyekundu, kijani, machungwa na njano. Zimetengenezwa kwa TPU.

Agiza hereni sasa

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Mnaweza kuchapisha jina la shamba langu kwenye hereni?

Ndiyo. Hereni zilizochapishwa hutengenezwa kwa oda – tutumie WhatsApp jina la shamba, namba na idadi unayohitaji.

Naweza kulipa nikipokea hereni?

Ndiyo. Lipa KSh 250 (KSh 1,000 kwa hereni zilizochapishwa) unapoagiza, kisha salio kwa M-Pesa unapochukua kwenye kituo chetu cha kuchukulia mizigo karibu nawe.

Nahitaji kifaa maalum kufunga hereni?

Ndiyo, applicator ya hereni. Applicator moja inatosha kwa mifugo yako yote.

Duka letu: Mkulima Jovial, Mfangano Trade Center Building, Ghorofa ya 3, Duka Na. T2A, Nairobi CBD – kwenye Mtaa wa Mfangano, jengo moja na Great Rift Sacco, karibu na East Matt Supermarket. Tuko wazi Jumatatu hadi Jumamosi, saa 2:30 asubuhi (8:30 am) hadi saa 12:00 jioni (6:00 pm). Jumapili tumefungwa.

Piga simu au WhatsApp: 0795 485 349. Tunasafirisha kote nchini ndani ya saa 24, na siku hiyo hiyo ndani ya Nairobi. Usafirishaji ndani ya Nairobi CBD ni bure, na tunafikisha oda yako kwa courier au matatu ya mizigo bila malipo – unalipa tu nauli ya mzigo hadi mji wako. Lipa kwa M-Pesa.

Kurasa zaidi kwa Kiswahili: orodha kamili ya bei · incubator · gas brooder · vyombo vya chakula na maji · trei za mayai · mifuko ya silage · hereni za mifugo · vifurushi vya kuanzia · mawasiliano

Read this page in English